Sanidi taarifa ya barua pepe kwa kutumia Web Config kutoka kwenye kompyuta kwenye mtandao wa kawaida.
Ingiza anwani ya IP ya mtandao wa kawaida kwenye kivinjari ili kufikia Web Config.
Teua kichupo cha Device Management > Email Notification.
Weka mada ya taarifa ya barua pepe.
Teua maudhui yanayoonyeshwa kwenye mada kutoka katika menyu mbili za kuvuta chini.
Ingiza anwani ya barua pepe ya kutuma barua ya taarifa.
Tumia A–Z a–z 0–9 ! # $ % & ' * + - . / = ? ^ _ { | } ~ @, na uingize vibambo kati ya vibambo 1 na 255.
Teua Standard au Additional kwa mitandao inayotumika kutuma kwa wapokeaji.
Teua lugha kwa ajili ya taarifa za barua pepe.
Teua kisanduku cha kuteua kwenye tukio unalotaka kupokea taarifa kulihusu.
Idadi ya Notification Settings kinaunganishwa kwenye idadi ya Email Address Settings.
Mfano:
Iwapo unataka taarifa itumwe kwenye anwani ya barua pepe ya nambari 1 katika Email Address Settings wakati kichapishi hakina karatasi, teua safu ya kisanduku cha uteuzi cha 1 katika mstari wa Paper out.
Bofya OK.
Thibitisha kwamba taarifa ya barua pepe itatumwa kwa kusababisha tukio.
Mfano: chapisha kwa kubainisha Chanzo cha K'tasi ambapo karatasi haijawekwa.