Kusanidi Kioleosura

Weka muda wa kukamilika kwa kazi za kuchapisha au lugha ya kuchapisha uliokabidhiwa kila kioleosura.

Kipengee kinaonyeshwa kwenye kichapishi kinachoambatana na PCL au PostScript.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Print kichupo > Interface Settings

  4. Teua kila kipengee.

    • Timeout Settings
      Weka muda kukwisha wa kazi za kuchapisha zilizotumwa moja kwa moja kupitia USB.
      Unaweza kuweka kati ya sekunde 5 na 300 kulingana na sekunde.
      Iwapo hutaki muda kukwisha, ingiza 0.
    • Printing Language
      Teua lugha ya kuchapisha kwa kila kiolesura cha USB au kiolesura cha mtandao.
      Unapoteua Auto, lugha ya kuchapisha hugunduliwa kiotomatiki na kazi cha kuchapisha zinazotumwa.
  5. Angalia mipangilio, na kisha ubofye OK.