Suluhisho
Uunganishaji mlalo (mtagusano wa pembe 90 kwa mwelekeo wa uchapishaji) unapoonekana, au shemu ya juu au ya chini imepakwa, pakia karatasi kwenye mwelekeo ufaao na utelezeshe miongozo ya kingo hadi kwenye kingo za karatasi.
Suluhisho
Usiweke zaidi ya upeo wa idadi ya karatasi uliotajwa kwa karatasi. Kwa karatasi tupu, usiweke zaidi ya mstari unaoonyeshwa na alama ya pembetatu kwenye mwongozo wa kingo.
Suluhisho
Weka karatasi katika eneo laini ili kuangalia iwapo imejikunja. Iwapo ndivyo, ilainishe.
Suluhisho
Angalia hali ya karatasi. Iwapo karatasi itaingiza maji, inakuwa na mawimbi au kujikunja ambako kunaweza kusababisha matatizo.
Suluhisho
Iwapo karatasi zimechafuka au kuchakaa mara kwa mara, jaribu kutumia karatasi mpya zilizofunguliwa.
Suluhisho
Wakati unachapisha katika karatasi nono, kichwa cha chapisho kiko karibu na eneo la uchapishaji na karatasi inaweza kuchafuliwa. Katika hali hii, wezeshga mpangilio wa kupunguza uchafu. Ukiwasha mpangilio huu, ubora wa uchapishaji unaweza kupungua au uchapishaji unaweza kuwa na kasi ya chini.
Paneli Dhibiti
Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa, na kisha uwezeshe Karatasi Nyembamba. Tazama skrini ya LCD ya kichapishi kwa chaguo za mpangilio.
Suluhisho
Iwapo bado karatasi imechafuka baada ya kuwezesha Karatasi Nyembamba, punguza uzito wa chapisho.
Suluhisho
Unapofanya uchapishaji wa pande 2 mwenyewe, hakikisha kwamba wino umekauka kabisa kabla ya kupakia karatasi upya.
Suluhisho
Wakati unatumia kipengele cha uchapishaji wa pande 2 na kuchapisha data ya uzito wa juu kama vile picha na grafu, weka uzito wa uchapishai kwa chini na muda wa kukauka kwa refu.