Kusafisha ADF

Wakati picha zilizonakiliwa au kutambazwa kutoka kwa ADF zimechafuka au za asili haziingii katika ADF ipasavyo, safisha ADF.

Muhimu:

Usiwahi kutumia pombe au thina kusafisha printa. Kemikali hizi zinaweza kuharibu printa.

  1. Fungua kifuniko cha ADF.

  2. Tumia kitambaa safi kilicho na maji kusafisha rola na ndani ya ADF.

    Muhimu:
    • Kutumia kitambaa kilichokauka kunawea kuharibu eneo la rola.

    • Tumia ADF baada ya rola kukauka.

  3. Funga kifuniko cha ADF.

    Bonyeza leva hadi kitoe sauti.

  4. Fungua kifuniko cha hati.

  5. Chukua kitambaa cha kusafisha kwenye kibeba kitambaa cha kusafisha.

  6. Tumia kitambaa cha kusafisha ili kusafisha sehemu ambayo imeonyeshwa kwenye mfano.

    Muhimu:
    • Iwapo eneo la kioo limekwamiliwa na grisi au nyenzo nyingine ngumu kuondoa, tumia kiasi kidogo cha kisafishaji kioo na kitambaa laini kuiondoa. Pangusa unyevu wote unaobakia.

    • Usibonyeze glasi kwa nguvu.

    • Kuwa makini usikwaruze au kuharibu glasi. Glasi iliyoharibika inaweza kupunguza ubora wa utambazaji.

  7. Rejesha kitambaa cha kusafisha kwenye kibeba kitambaa cha kusafisha.

  8. Funga kifuniko cha hati.