> Kutatua Matatizo > Kichapishi Hakifanyi Kazi Inavyotarajiwa > Msimbo wa Hitilafu kwenye Menyu ya Hali

Msimbo wa Hitilafu kwenye Menyu ya Hali

Ikiwa kazi haitafanikiwa kukamilika, kagua msimbo wa hitilafu ulioonyeshwa kwenye historia ya kila kazi. Unaweza kuangalia hitialfu kwa kuteua Kazi/Hali > Hali ya Kazi. Angalia jedwali linalofuata ili upate tatizo na suluhisho lake.

Msimbo

Tatizo

Suluhisho

001

Bidhaa ilizimwa kwa sababu ya tatizo la nishati.

-

101

Kumbukumbu imejaa.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa kazi ya kuchapisha.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

102

Uchapishaji ulioainishwa umeshindikana kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa kazi ya kuchapisha. Iwapo unataka kutumia mbinu hizi, jaribu nakala moja kwa wakati mmoja.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

103

Ubora wa uchapishaji umepungua kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Iwapo hutaki kupunguza ubora wa chapisho, jaribu mbinu zifuatazo ili kupunguza ukubwa wa kazi ya uchapishaji.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

104

Uchapishaji wa kinyume umeshindikana kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Iwapo hutaki chapisho katika kinyume, jaribu mbinu zifuatazo ili kupunguza ukubwa wa kazi ya uchapishaji.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

106

Haiwezi kuchapisha kutoka kwenye kompyuta kwa sababu ya mipangilio ya kudhibiti ufikiaji.

Wasiliana na msimamizi wako wa kichapishi.

107

Uhalalishaji wa mtumiaji umeshindikana. Kazi imekatishwa.

  • Hakikisha kuwa jina la mtumiaji na nywila ni sahihi.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Mipangilio ya Usalama > Fikia Vidhibiti. Wezesha kitendaji cha kuzuia mtumiaji, na kisha uruhusu kazi bila maelezo ya uhalalishaji.

108

Data ya siri ya kazi ilifutwa wakati kichapishi kilizimwa.

-

109

Faksi iliyopokewa ilikuwa imefutwa tayari.

-

110

Kazi ilichapishwa kwenye upande mmoja tu kwa sababu karatasi iliyopakiwa haikubali uchapishaji wa pande mbili.

Ikiwa unataka kutekeleza uchapishaji wa pande 2, pakia karatasi ambazo inakubali uchapishaji wa pande 2.

111

Kumbukumbu iliyopo inapungua nafasi.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa kazi ya kuchapisha.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

120

Haiwezi kuwasiliana na seva iliyounganishwa kwa kutumia jukwaa wazi.

Hakikisha hakuna makosa kwenye seva au mtandao.

130

Uchapishaji ulioainishwa umeshindikana kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa kazi ya kuchapisha. Iwapo unataka kutumia mbinu hizi, jaribu nakala moja kwa wakati mmoja.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

131

Uchapishaji wa kinyume umeshindikana kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Iwapo hutaki chapisho katika kinyume, jaribu mbinu zifuatazo ili kupunguza ukubwa wa kazi ya uchapishaji.

  • Punguza ubora na mwonekano wa chapisho.

  • Badilisha mpangilio wa umbizo.

  • Punguza idadi ya picha, herufi au fonti zinazotumiwa kwenye kazi ya kuchapisha.

132

Haiwezi kuchapisha kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa data ya kuchapisha.

  • Badilisha saizi ndogo ya karatasi.

  • Rahisisha data kwa kupunguza idadi ya picha kwenye data ya kuchapisha au kupunguza idadi ya aina za fonti.

133

Haiwezi kuchapisha kwenye pande 2 kwa sababu ya ukosefu wa kumbukumbu inayopatikana. Upende mmoja tu utachapishwa.

Jaribu mbinu zilizo hapa chini ili kupunguza ukubwa wa data ya kuchapisha.

  • Badilisha saizi ndogo ya karatasi.

  • Rahisisha data kwa kupunguza idadi ya picha kwenye data ya kuchapisha au kupunguza idadi ya aina za fonti.

141

Kosa kwenye HDD ya kichapishi. Kazi imekatishwa.

Wasiliana na auni ya Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili kubadilisha HDD.

151

Uchapishaji hautekelezwi kwa sababu jina la mtumiaji la kuingia na jina la mtumiaji linalohusiana na kazi ya siri hayalingani.

Hakikisha umeingia kwa jina la mtumiaji sawa na jina la mtumiaji linalohusiana na kazi ya siri.

161

Udhibiti wa hesabu ya kurasa umewekwa katika Epson Print Admin Serverless. Haikuweza kuchapisha kwa sababu idadi ya kurasa zilizosalia haitoshi.

Wasiliana na msimamizi wako wa mfumo.

201

Kumbukumbu imejaa.

  • Chapisha faksi zilizopokewa kutoka Hali ya Kazi katika Kazi/Hali.

  • Futa faksi zilizopokewa katika kisanduku pokezi kutoka Hali ya Kazi katika Kazi/Hali.

  • Ikiwa unatuma faksi ya rangi moja katika mahali pamoja, unaweza kuituma kwa kutumia Utumaji wa Moja kwa Moja.

  • Gawanya hati zako halisi ziwe mbili au zaidi ili uzitume kwa makundi kadhaa.

202

Laini imetenganishwa na mashine ya mpokeaji.

Subiri kwa muda na kisha ujaribu tena.

203

Bidhaa haiwezi kugundua toni ya kudayo.

  • Hakikisha kwamba kebo ya simu imeunganishwa vizuri na laini ya simu inafanya kazi.

  • Wakati printa imeungannishwa kwenye PBX au adapta ya temino, badilisha mpangilio wa Aina ya Laini kwa PBX.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Ugunduaji Mlio wa kupiga Simu, na kisha ulemaze mpangilio wa toni ya kudayo.

204

Mashine ya mpokeaji ina shughuli.

  • Subiri kwa muda na kisha ujaribu tena.

  • Angalia nambari ya faksi ya mpokeaji.

205

Mashine ya mpokeaji haijibu.

Subiri kwa muda na kisha ujaribu tena.

206

Kebo ya simu imeunganishwa vibaya kwenye LINE na kituo cha EXT. cha bidhaa.

Kagua muunganisho wa kituo cha LINE na kituo cha EXT. cha printa.

207

Bidhaa haijaunganishwa kwenye laini ya simu.

Unganisha kebo ya simu kwenye laini ya simu.

208

Faksi haikuweza kutumwa kwa baadhi ya wapokeaji waliobainishwa.

Chapisha Kumbukumbu ya Faksi au ripoti ya Upitishaji wa Mwisho ya faksi za awali kutoka kwa Ripoti ya Faksi katika Hali ya faksi ili ukagua tatizo la mafikio. Wakati mpangilio wa Hifadhi Data ya Kushindwa umewezeshwa, unaweza kutuma faksi tena kutoka Hali ya Kazi katika Kazi/Hali.

301

Hakuna nafasi ya kutosha ya kumbukumbu ya kuhifadhi data katika kifaa cha kumbukumbu.

  • Ongeza nafasi ya hifadhi katika kifaa cha kumbukumbu.

  • Punguza idadi ya hati.

  • Punguza mwonekano wa kuchanganua au ongeza mgao wa mfinyazo ili upunguze ukubwa wa picha iliyochanganuliwa.

302

Kifaa cha kumbukumbu kimelindwa dhidi ya kuandikwa.

Leza ulinzi wa kuandika kwenye kifaa cha kumbukumbu.

303

Hakuna folda iliyoundwa ili kuhifadhi picha iliyochanganuliwa.

Ingiza kifaa kingine cha kumbukumbu.

304

Kifaa cha kumbukumbu kimeondolewa.

Ingiza upya kifaa cha kumbukumbu.

305

Hitilafu imetokea wakati wa kuhifadhi data kwenye kifaa cha kumbukumbu.

Ikiwa kifaa cha nje kinafikiwa kutoka kwenye kompyuta, subiri kwa muda na kisha ujaribu tena.

306

Kumbukumbu imejaa.

Subiri hadi kazi nyingine zinazoendelea zikamilike.

307

Ukubwa wa picha iliyotambazwa huzidisha kiwango cha juu zaidi. (Tambaza kwenye Kifaa cha Kumbukumbu)

Punguza mwonekano wa kuchanganua au ongeza mgao wa mfinyazo ili upunguze ukubwa wa picha iliyochanganuliwa.

311

Hitilafu ya DNS imetokea.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > TCP/IP, na kisha ukague mipangilio ya DNS.

  • Kagua mipangilio ya DNS ya seva, kompyuta, au eneo la ufikiaji.

312

Hitilafu ya uhalalishaji imetokea.

Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > Seva ya Barua pepe > Mipangilio ya Seva, na kisha ukague mipangilio ya seva.

313

Hitilafu ya mawasiliano imetokea.

  • Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > Seva ya Barua pepe > Mipangilio ya Seva ili ukague kama mipangilio ya seva ya barua pepe. Unaweza kuangalia sababu ya kosa kwa kufanya ukaguzi wa muunganisho.

  • Mbinu ya uhalalishaji ya mipangilio na seva ya barua pepe huenda isilingane. Unapochagua Zima kama mbinu ya uhalalishaji, hakikisha mbinu ya uhalalishaji ya seva ya barua pepe imewekwa kuwa Hakuna.

314

Ukubwa wa data unazidisha upeo wa ukubwa kwa faili zilizoambatishwa.

  • Ongeza mpangilio wa Upeo wa Ukubwa wa Kiambatisho katika mipangilio ya uchanganuzi.

  • Punguza mwonekano wa kuchanganua au ongeza mgao wa mfinyazo ili upunguze ukubwa wa picha iliyochanganuliwa.

315

Kumbukumbu imejaa.

Jaribu tena baada ya kazi nyingine zinazoendelea zikamilike.

316

Hitilafu ya usimbaji wa barua pepe imetokea.

  • Hakikisha mpangilio wa cheti cha usimbaji ni sahihi.

  • Hakikisha mpangilio wa saa wa kichapishi ni sahihi.

317

Hitilafu ya sahihi ya barua pepe imetokea.

  • Hakikisha mpangilio wa utiaji wa sahihi kwenye cheti ni sahihi.

  • Hakikisha mpangilio wa saa wa kichapishi ni sahihi.

318

Hitilafu ya uzuiaji wa kikoa imetokea.

Wasiliana na msimamizi wako ili kuangalia iwapo kikoa cha ufikio wa barua pepe yako umezuiwa.

321

Hitilafu ya DNS imetokea.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > TCP/IP, na kisha ukague mipangilio ya DNS.

  • Kagua mipangilio ya DNS ya seva, kompyuta, au eneo la ufikiaji.

322

Hitilafu ya uhalalishaji imetokea.

Angalia mipangilio ya Eneo.

323

Hitilafu ya mawasiliano imetokea.

  • Angalia mipangilio ya Eneo.

  • Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

324

Faili yenye jina laka hilo tayari ipo katika folda iliyobainishwa.

  • Futa faili yenye jina sawa.

  • Badilisha kiambishi awali cha jina la faili katika Mipanilio ya Faili.

325

326

Hakuna nafasi ya kutosha ya kuhifadhi katika folda iliyobainishwa.

  • Ongeza nafasi ya hifadhi katika folda iliyobainishwa.

  • Punguza idadi ya hati.

  • Punguza mwonekano wa kuchanganua au ongeza mgao wa mfinyazo ili upunguze ukubwa wa picha iliyochanganuliwa.

327

Kumbukumbu imejaa.

Subiri hadi kazi nyingine zinazoendelea zikamilike.

328

Mafikio hayakuwa sahihi au mafikio hayapo.

Angalia mipangilio ya Eneo.

329

Ukubwa wa picha iliyotambazwa huzidisha kiwango cha juu zaidi. (Kutambaza kwenye Kabrasha la Mtandao au Seva ya FTP)

Punguza mwonekano wa kuchanganua au ongeza mgao wa mfinyazo ili upunguze ukubwa wa picha iliyochanganuliwa.

330

Hitilafu ya muunganisho salama wa FTPS/FTPS imetokea.

  • Angalia eneo kwenye mipangilio ya ufikio.

  • Endesha Web Config, na kisha usasishe cheti cha kina.

  • Endesha Web Config, na kisha ulete au usasishe cheti cha CA.

Iwapo hitilafu hiyo haiwezi kufutwa, zima uthibitshaji wa cheti kwenye mipangilio ya ufikio.

331

Kosa la mawasiliano limetokea.

Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

332

Hakuna nafasi ya kutosha ya kuhifadhi inayopatikana ili kuhifadhi picha iliyochanganuliwa katika hifadhi mwishilio.

Punguza idadi ya hati.

333

Mwishilio haukuweza kupatikana kwa sababu maelezo ya mwishilio yalipakiwa kwenye seva kabla ya kutuma picha iliyochanganuliwa.

Teua tena mwishilio.

334

Hitilafu imetokea wakati wa kutuma picha iliyochanganuliwa.

-

341

Hitilafu ya mawasiliano imetokea.

  • Angalia miunganisho ya printa na kompyuta. Ikiwa unaunganisha kwenye mtandao, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

  • Hakikisha kwamba Document Capture Pro imesakinishwa kwenye kompyuta.

350

Hitilafu ya cheti cha FTPS/HTTPS imetokea.

  • Hakikisha kwamba mipangilio ya tarehe/saa na utofauti wa saa ni sahihi.

  • Endesha Web Config, na kisha usasishe cheti cha kina.

  • Endesha Web Config, na kisha ulete au usasishe cheti cha CA.

Iwapo hitilafu hiyo haiwezi kufutwa, zima uthibitshaji wa cheti kwenye mipangilio ya ufikio.

401

Hakuna nafasi ya kutosha ya kumbukumbu ya kuhifadhi data katika kifaa cha kumbukumbu.

Ongeza nafasi ya hifadhi katika kifaa cha kumbukumbu.

402

Kifaa cha kumbukumbu kimelindwa dhidi ya kuandikwa.

Leza ulinzi wa kuandika kwenye kifaa cha kumbukumbu.

404

Kifaa cha kumbukumbu kimeondolewa.

Ingiza upya kifaa cha kumbukumbu.

405

Hitilafu imetokea wakati wa kuhifadhi data kwenye kifaa cha kumbukumbu.

  • Ingiza upya kifaa cha kumbukumbu.

  • Tumia kifaa tofauti cha kumbukumbu ambacho folda yako imeundwa kwa kutumia kitendaji cha Unda Folda ili Kuhifadhi.

411

Hitilafu ya DNS imetokea.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > TCP/IP, na kisha ukague mipangilio ya DNS.

  • Kagua mipangilio ya DNS ya seva, kompyuta, au eneo la ufikiaji.

412

Hitilafu ya uhalalishaji imetokea.

Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > Seva ya Barua pepe > Mipangilio ya Seva, na kisha ukague mipangilio ya seva.

413

Hitilafu ya mawasiliano imetokea.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > Seva ya Barua pepe > Mipangilio ya Seva ili ukague kama mipangilio ya seva ya barua pepe. Unaweza kuangalia sababu ya kosa kwa kufanya ukaguzi wa muunganisho.

  • Mbinu ya uhalalishaji ya mipangilio na seva ya barua pepe huenda isilingane. Unapochagua Zima kama mbinu ya uhalalishaji, hakikisha mbinu ya uhalalishaji ya seva ya barua pepe imewekwa kuwa Hakuna.

  • Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

421

Hitilafu ya DNS imetokea.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > TCP/IP, na kisha ukague mipangilio ya DNS.

  • Kagua mipangilio ya DNS ya seva, kompyuta, au eneo la ufikiaji.

422

Hitilafu ya uhalalishaji imetokea.

Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza, na kisha ukague mipangilio ya kabrasha iliyoteuliwa kwenye Mfikio.

423

Hitilafu ya mawasiliano imetokea.

  • Chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili ukague kama printa imeunganishwa kwenye mtandao.

  • Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza, na uteue kwenye kisanduku kilichosajiliwa. Kisha, angalia mpangilio wa kabrasha kwenye Hifadhi/Sambaza Mfikio.

425

Hakuna nafasi ya kutosha ya kuhifadhi inayopatikana katika kabrasha la mafikio ya kusambaza.

Ongeza nafasi ya hifadhi katika kabrasha la mafikio ya kusambaza.

428

Mafikio hayakuwa sahihi au mafikio hayapo.

Donoa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza, na uteue kwenye kisanduku kilichosajiliwa. Kisha, angalia mpangilio wa kabrasha kwenye Hifadhi/Sambaza Mfikio.

501

Haiwezi kutumia kipengele cha hifadhi.

Angalia ruhusa za mtumiaji kutoka kwenye Web Config.

502

Eneo la hifadhi limejaa.

Futa kazi zisizo muhimu zilizohifadhiwa kutoka kwenye paneli dhibiti au Web Config.

504

Idadi ya faili imefikia kikomo cha juu zaidi.

Futa kazi zisizo muhimu zilizohifadhiwa kutoka kwenye paneli dhibiti au Web Config.

505

Kosa la kusoma/kuandika limetokea kwenye hifadhi.

Wasiliana na usaidizi wa Epson.