Unapowezesha udhibiti wa ufikiaji, mtumiaji aliyesajiliwa pekee ndiye ataweza kutumia kichapishi.
Fikia Usanidi wa Wavuti na uteue kichupo cha Product Security > Access Control Settings > Basic.
Teua Enables Access Control.
Iwapo utateua Allow printing and scanning without authentication information from a computer, unaweza kuchapisha au kutambaza kutoka kwenye viendeshi visivyosanidiwa na maelezo ya uhalalishaji. Sanidi unapotaka kudhibiti kitendo kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi pekee na uruhusu uchapishaji na utambazaji kutoka kwenye kompyuta.
Bofya OK.
Ujumbe wa ukamilisho unaonyeshwa baada ya muda fulani.
Thibitisha kwamba ikoni kama vile nakili na utambaze zimelemazwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.