Ili kutumia Document Capture Pro Server, sanidi ifuatavyo.
Fikia Web Config na uteue kichupo cha Scan/Copy > Document Capture Pro.
Teua Server Mode kwa Mode.
Ingiza anwani ya seva kwa Document Capture Pro Server iliyosakinishwa kwayo kwa Server Address.
Ingiza kati ya vibambo 2 hadi 255 vya IPv4, IPv6, jina la mpangishi au umbizo la FQDN. Kwa umbizo la FQDN, unaweza kutumia vibambo vya herufi na tarakimu kwenye ASCII (0x20–0x7E) na “- ” isipokuwa katika mwanzoni na mwishoni mwa anwani.
Bofya OK.
Mtandao unaunganishwa upya, na kisha mipangilio inawezeshwa.