Mpangilio wa Nakala na Seti

Bainisha idadi ya nakala na seti ngapi za kuchapisha kwa kila kikundi. Unaweza kuhifadhi hadi vikundi 60. Unaweza kuingiza hadi nakala 9999 na seti 99.

A: Nakala

B: Seti

Kwa mfano, iwapo ulitaka kuchapisha vijitabu vya madarasa manne (Darasa la 1: wanafunzi 30, Darasa la 2: wanafunzi 31, Darasa la 3: wanafunzi 32, Darasa la 4: wanafunzi 30) kwa shule, utaweka mipangilio ifuatayo.

-

Kikundi 1

Kikundi 2

Kikundi 3

Kikundi 4

Darasa

Darasa la 1

Darasa la 2

Darasa la 3

Darasa la 4

Nakala×Seti

30×1

31×1

32×1

30×1

Unaweza pia kuweka mipangilio ifuatayo kwa sababu idadi ya wanafunzi ni sawa kwa darasa la 1 na 4.

-

Kikundi 1

Kikundi 2

Kikundi 3

Darasa

Darasa la 1 na Darasa la 4

Darasa la 2

Darasa la 3

Nakala×Seti

30×2

31×1

32×1