Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma (WPS)

Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.

  • Kipanga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).

  • Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Ikiwa huwezi kupata kitufe au unasanidi kwa kutumia programu, tazama hati iliyotolewa kwa kipanga njia pasiwaya.

  1. Donoa kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Donoa Kipangishi njia.

  3. Donoa Anza Kusanidi.

  4. Donoa Usanidi wa Wi-Fi.

    Iwapo umeweka mipangilio ya Etherneti, angalia ujumbe kisha udonoe Ndiyo.

  5. Donoa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma(WPS).

  6. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

    Ukitaka kuangalia hali ya muunganisho wa mtandao ya kichapishi baada ya kukamilisha kusanidi, angalia kiungo cha maelezo husiani kilicho hapa chini kwa maelezo.

    Kumbuka:

    Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanga njia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.