Kuweka Mipangilio ya Usambazaji ili Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji hadi eneo, anwani ya barua pepe, folda za pamoja au mashine nyingine ya faksi kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa. Ukiweka mipangilio ya kusambaza faksi zilizopokewa, kwanza ongeza anwani inayosambazwa kwenye orodha ya anwani. Ili kusambaza kwa anwani ya barua pepe, unahitaji pia kusanidi mipangilio ya seva ya barua pepe kabla.

Kusanidi Seva ya Barua

Kuweka Kabrasha Lililoshirikiwa La Mtandao

Kufanya Waasiliani Kupatikana

Kabla ya kutumia kipengele cha kusambaza na kusambaza faksi zilizopokewa kwa muda uliobainishwa, hakikisha mipangilio ya kichapishi ya Tarehe/Saa na Utofauti wa Saa ni sahihi. Fikia menyu kutoka kwa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Mipangilio ya Tarehe/Saa.

Hati za rangi haziwezi kusambazwa kwenye mashine nyingine ya faksi. Huchakatwa kama hati ambazo zilishindwa kusambazwa.

Kumbuka:
  • Kando na kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, unaweza kutumia Web Config kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi. Teua kichupo cha Fax > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, teua nambari ya kisanduku cha siri na kisha uteue Edit na uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

  • Unaweza kuchapisha na/au kuhifadhi faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja. Weka mipangilio kwenye skrini ya Edit iliyotajwa hapa juu.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti yakichapishi, kisha uteue Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.

  2. Teua Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, kisha udonoe kwenye kisanduku ambacho hakijasajiliwa chini ya Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  3. Teua kikasha cha Jina na uingize jina unalotaka kusajili.

  4. Teua kikasha cha Hali ili kuunda mpangilio wa masharti.

    • Ul'shaji wa N'ari ya Faksi ya Mtumaji: iwapo nambari ya faksi inayoingia inalingana na masharti uliyoteua kwenye kipengee hiki, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Teua mashart ya Ul'shaji wa N'ari ya Faksi ya Mtumaji na uingize nambari ya faksi (idadi ya juu ya dijiti 20) kwa kuteua kikasha cha Nambari ya Faksi.
    • Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO): iwapo anwani ndogo (SUB) inawiana vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO) na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Anwani ndogo(NDOGO).
    • Ulinganishaji kamili wa nywila: iwapo nenosiri (SID) limewianishwa vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Ulinganishaji kamili wa nywila na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Nywila(SID).
    • Wakati wa Kupokea: kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa wakati wa kipindi maalum cha muda.
      Wezesha mpangilio wa Wakati wa Kupokea na kisha uweke muda katika Muda wa Kuanza na Muda wa Mwisho.
  5. Teua Hifadhi/Sambaza Mfikio, na kisha uweke mipangilio ya eneo la kusambazia.

    Teua Sambaza.

    Teua Ndiyo. Ili uchapishe hati kiotomatiki wakati unazisambaza, chagua Ndiyo na Uchapishe badala yake.

    Teua Mfikio > Ongeza Ingizo, kisha uteue maeneo ya kusambazia kutoka kwenye orodha yako ya waasiliani. Unaweza kubainisha anwani ya usambazaji.

    Ukimaliza kuchagua anwani za usambazaji, gusa Funga.

    Hakikisha kwamba anwani ya usambazaji uliyochagua ni sahihi, na kisha uchague Funga.

    Katika Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana, chagua kama unataka kuchapisha hati zilizopokewa au kuzihifadhi katika Kisanduku pokezi ya kichapishi wakati usambazaji unakosa kufaulu.

    Muhimu:

    Wakati Kisanduku pokezi au kisanduku cha siri kimejaa, upokeaji wa faksi unalemazwa. Unastahili kufuta hati kwenye kisanduku pokezi punde tu zinapoangaliwa. Idadi ya nyaraka ambazo zilishindwa kusambaza imeonyeshwa kwenye katika skrini ya nyumbani, kwa kuongezea kwenye kazi zingine zisizochakatwa.

  6. Teua Funga ili ukamilishe Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza Mfikio.

    Kumbuka:

    Unaweza kuweka kichapishi kitume barua pepe kwa watu unaotaka kuwaarifu kuhusu matokeo ya usambazaji wa faksi wakati mchakato wa usambazaji ukikamilika. Ilivyo muhimu, teua Taarifa za Barua pepe, weka michakato na kisha uteue eneo unapotaka kutuma arifa kutoka kwenye orodha ya waasiliani.

  7. Teua Sawa hadi urejee kwenye skrini ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza ili kukamilisha Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  8. Teua kisanduku kilichosajiliwa ambacho ulifanya mpangilio wa masharti, na kisha uteue Wezesha.

Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya uhifadhi na usambazaji wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

Kumbuka:
  • Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya usambazaji wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

  • Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao au anwani ya barua pepe kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha iliyochanganuliwa hadi kwa mwishilio katika hali ya uchanganuzi. Teua Changanua > Barua pepe, au Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye skrini ya nyumbani, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.