Kusanidi Nenosiri la Msimamizi kutoka kwa Mtandao wa Ziada

Unaweza kuweka nenosiri la msimamizi ukitumia Web Config kutoka kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye mtandao wa ziada.

  1. Ingiza anwani ya IP ya mtandao wa ziada kwenye kivinjari ili kufikia Web Config.

  2. Teua kichupo cha Product Security > Change Administrator Password.

  3. Ingiza nenosiri kwenye New Password na Confirm New Password. Ingiza jina la mtumiaji, iwapo ni muhimu.

    Iwapo ungependa kubadilisha nenosiri hadi mpya, ingiza nenosiri la sasa.

  4. Teua OK.

    Kumbuka:

    Ili kuweka au kubadilisha vipengee vya menyu vilivyofungwa, bofya Administrator Login, kisha uingize nenosiri la msimamizi.