Unaweza kuweka nenosiri la msimamizi kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Wakati sera ya nenosiri inapatikana, ingiza nenosiri linalofikia mahitaji.
Unaweza kuweka mipangilio ya sera ya nenosiri kwa kuteua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Mipangilio ya Usalama > Sera ya Nywila.
Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao > Mipangilio ya Usalama > Mipangilio ya Msimamizi.
Teua Nenosiri la Msimamizi > Sajili.
Ingiza nenosiri jipya.
Ingiza nenosiri tena.
Unaweza kubadilisha au kufuta nenosiri la msimamizi unapoteua Badilisha au Rejeza Mipangilio Chaguo-msingi kwenye skrini ya Nenosiri la Msimamizi na uweke nenosiri la msimamizi.