Kuweka Mipangilio ya Kuhifadhi ili Kupokea Faksi kwa Masharti Yaliyobainishwa

Unaweza kuweka mipangilio ya kuhifadhi faksi zinazopokewa kwenye kikasha pokezi na kifaa cha kumbukumbu ya nje kutoka kwa mtumaji aliyebainishwa au muda uliobainishwa. Kuhifadhi faksi kwenye kisanduku cha siri au kikasha pokezi kuhurushu kuthibitisha maudhui ya faksi zilizopokelewa kwa kutazama kwenye skrini ya kichapishi cha LCD kabla ya kichapishi kuchapisha faksi.

Kabla ya kutumia kipengele cha kuhifadhi faksi zilizopokewa kwa muda uliobainishwa, hakikisha mipangilio ya kichapishi ya Tarehe/Saa na Utofauti wa Saa ni sahihi. Fikia menyu kutoka kwa Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Mipangilio ya Tarehe/Saa.

Kumbuka:
  • Kando na kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, unaweza kutumia Web Config kuweka mipangilio ya kuhifadhi ili kupokea faksi. Teua kichupo cha Fax > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, teua nambari ya kisanduku cha siri na kisha uteue Edit na uweke mipangilio ya eneo la kuhifadhia.

  • Unaweza pia kuchapisha na/au kusambaza faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja. Weka mipangilio kwenye skrini ya Edit iliyotajwa hapa juu.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti yakichapishi, kisha uteue Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.

  2. Teua Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Masharti ya Hifadhi/Sambaza, kisha udonoe kwenye kisanduku ambacho hakijasajiliwa chini ya Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  3. Teua kikasha cha Jina na uingize jina unalotaka kusajili.

  4. Teua kikasha cha Hali ili kuunda mpangilio wa masharti.

    • Ul'shaji wa N'ari ya Faksi ya Mtumaji: iwapo nambari ya faksi inayoingia inalingana na masharti uliyoteua kwenye kipengee hiki, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Teua mashart ya Ul'shaji wa N'ari ya Faksi ya Mtumaji na uingize nambari ya faksi (idadi ya juu ya dijiti 20) kwa kuteua kikasha cha Nambari ya Faksi.
    • Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO): iwapo anwani ndogo (SUB) inawiana vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Uli'shaji kamili anwani ndogo (NDOGO) na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Anwani ndogo(NDOGO).
    • Ulinganishaji kamili wa nywila: iwapo nenosiri (SID) limewianishwa vilivyo, kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa.
      Wezesha mpangilio wa Ulinganishaji kamili wa nywila na uingize nenosiri kwa kuteua kikasha cha Nywila(SID).
    • Wakati wa Kupokea: kichapishi huhifadhi na kusambaza faksi zilizopokewa wakati wa kipindi maalum cha muda.
      Wezesha mpangilio wa Wakati wa Kupokea na kisha uweke muda katika Muda wa Kuanza na Muda wa Mwisho.
  5. Teua Hifadhi/Sambaza Mfikio kisha uweke mipangilio ya eneo unapolenga, kisanduku, na au kifaa cha kumbukumbu ya nje.

    • Kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye Kisanduku pokezi au kisanduku cha siri:
      Teua Hifadhi kwenye Kasha la Faksi.
      Donoa Hifadhi kwenye Kasha la Faksi ili kuweka hii kwa Washa.
      Chagua kisanduku cha kuhifadhi hati.
    • Kuhifadhi faksi zilizopokewa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha nje:
      Ingiza kifaa cha kumbukumbu kwenye lango la USB la kiolesura la nje la kichapishi.
      Teua Hifadhi kwenye Kumbukumbu.
      Donoa Hifadhi kwenye Kumbukumbu ili kuweka hii kwa Washa.
      Angalia ujumbe unaoonyeshwa, na kisha uguse Unda.
      Kabrasha la kuhifadhi nyaraka zilizopokewa huundwa katika kifaa cha kumbukumbu.
      Muhimu:

      Hati zilizopokewa uhifadhiwa kwa muda kwenye kumbukumbu ya kichapishi kabla ya nyaraka kuhifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichounganishwa kwenye kichapishi. Kwa sababu hitilafu ya kumbukumbu kujaa hulemaza kutuma na kupokea faksi, weka kifaa cha kumbukumbu kikiwa kimeunganishwa kwenye kichapishi.

    Kumbuka:

    Ili kuchapisha faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja, donoa Chapisha ili uweke hii iwe Washa.

  6. Teua Funga ili ukamilishe Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza Mfikio.

    Kumbuka:

    Unaweza kuweka kichapishi kitume barua pepe kwa watu unaotaka kuwaarifu kuhusu matokeo ya kuhifadhi faksi wakati mchakato wa uhifadhi ukikamilika. Ilivyo muhimu, teua Taarifa za Barua pepe, weka michakato na kisha uteue eneo unapotaka kutuma arifa kutoka kwenye orodha ya waasiliani.

  7. Teua Sawa hadi urejee kwenye skrini ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza ili kukamilisha Masharti ya Hifadhi/Sambaza.

  8. Teua kisanduku kilichosajiliwa ambacho ulifanya mpangilio wa masharti, na kisha uteue Wezesha.

Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya uhifadhi wa masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.