Unaweza kuchapisha maelezo kama vile jina la mtumiaji na tarehe ya kuchapisha kwenye vijajuu na vijachini.

Kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi, Chaguo Zaidi bofya Vipengele vya Taswira fifi, na kisha uteue kisanduku cha kuteua cha Kijajuu/Kijachini.
Teua Mipangilio, teua vipengee unavyotaka kuchapisha kisha ubofye OK.
Ili kubainisha nambari ya ukurasa wa kwanza, teua Nambari ya Ukurasa kutoka katika nafasi unayotaka kuchapisha katika kijajuu au kijachini, kisha uteue nambari kwenye Nambari ya kuanzia.
Iwapo unataka kuchapisha matini kwenye kijajuu au kijachini, teua nfafasi unayotaka kuchapisha na kisha uteue Matini. Ingiza matini unayotaka kuchapisha kwenye sehemu ya kuingiza matini.
Weka vipengee hivyo vingine kwenye Kuu, Kukamilisha au vichupo vya Chaguo Zaidi inavyohitajika, kisha ubofye SAWA.
Bofya Chapisha.