Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Huwezi kubadilisha mipangilio iliyozuiwa na msimamizi wako.
Rekebisha sauti.
Nyamazisha
Teua Washa ili kunyamazisha sauti kama zile zitolewazo na Ubonyezaji Kitufe.
Hali ya Kawaida
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.
Hali Tulivu
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe kwenye Hali Tulivu.
Teua Washa ili kutambua kosa la karatasi inayoingizwa mara mbili unapotambaza kwa ADF.
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Teua Washa ili kurudi kutoka kwenye modi ya kulala (modi ya kuhifadhi nishati) kwa kudonoa paneli ya mguso. Wakati hii imezimwa, unahitaji kubonyeza kitufe cha nishati kwenye paneli dhibiti ili kuwasha kichapishi. Kuzima kipengele hiki huzuia operesheni zozote zisizo kusudiwa zilizosababishwa na vifaa vya nje kugusa skrini. Pia unaweza kuweka kipindi cha muda ambacho kipengele hiki kimewashwa.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima saa cha Kuzima Nishati kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha LINE kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Mpangilio huu huzimwa wakati bodi ya hairi ya ethaneti au faksi imesakinishwa.
Tarehe/Saa
Ingiza tarehe na saa ya sasa.
Muda wa Kuokoa Mwanga wa Mchana
Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.
Utofauti wa Saa
Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).
Teua nchi au eneo ambalo unatumia kichapishi chako. Iwapo utabadilisha nchi au eneo, mipangilio yako ya faksi inarejea kwa chaguo-msingi na lazima uiteue tena.
Bainisha menyu ya kwanza inayoonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati kichapishi kinawaka na Muda wa Shughuli Umeisha imewezeshwa.
Badillisha muundo wa ikoni kwenye skrini ya LCD. Pia unaweza kuongeza, kuonmdoa, na kuhamisha ikoni.
Badilisha rangi ya mandharinyuma ya skrini ya LCD.
Pia unaweza kuteua taswira ya mandharinyuma kuitoka kwenye kifaa cha kumbukumbu. Umbizo la JPEG pekee linaauniwa.
Teua Washa ili kurejesha skrini ya kwanza wakati hakuna operesheni imetekelezwa kwa muda uliobainishwa. Wakati vizuizi vya mtumiaji vimewekwa na hakuna operesheni zinatekelezwa kwa muda uliobainishwa, unaondolewa na kurejeshwa kwenye skrini ya kwanza. Wakati uchapishaji umesitishwa kutoka kwenye kiwambo cha hali au kitufe cha kukatisha au kusitisha, na kisha hakuna operesheni zilizotekelezwa kwa muda uliobainishwa, uchapishaji huendelea kiotomatiki. Iwapo utateua Zima kwa kipengele hiki, haiendelei kiotomatiki baada ya kusitishwa kwa uchapishaji.
Weka Washa ili ionyeshe ujumbe wa uthibitishaji unaouliza kama unataka kuendelea na uchapishaji wakati kazi ya uchapishaji ya kijivu inahesabiwa kama kazi ya uchapishaji ya rangi.
Teua maelezo chaguo-msingi unayotaka kuonyesha unapodonoa Kazi/Hali.
Teua Washa ili kuwezesha athari za uhuishaji unapobadili skrini. Iwapo utateua Zima, kubadili skrini ni rahisi.
ADF na glasi ya kitambazaji zina sensa ambazo hutambua otomatiki ukubwa wa karatasi. Hata hivyo, kutokana na mifano ya sensa, ukubwa sawa hauwezi kutambuliwa, na karatasi ya ukubwa wa K, ambayo inatumika zaidi China, haiwezi kutambuliwa sahihi katika hali ya awali ya kichapishi. Teua Kipaumbele cha Ukubwa wa K iwapo kila mara huwa unatumia ukubwa wa karatasi wa K. Ukubwa asili utatambuliwa kama ukubwa wa K badala ya ukubwa unaokaribia. Kutegemea ukubwa na mwelekeo wa karatasi, inaweza kugunduliwa kama ukubwa mwingine unaokaribia. Pia, ukubwa wa K unaweza kukosa kugunduliwa kutegemea kazi unayotumia. Kwa mfano, unapotambaza na kuhifadhi kwenye kompyuta kwa kutumia programu hiyo, kama au la ukubwa wa K unaweza kutambuliwa otomatiki kunategemea tabia ya programu hiyo.