Kuweka Mipangilio ya Usambazaji ili Kupokea Faksi

Unaweza kuweka mipangilio ya usambazaji hadi maeneo matano, anwani za barua pepe, folda za pamoja na/au mashine nyingine ya faksi licha ya mtumiaji au muda. Ukiweka mipangilio ya kusambaza faksi zilizopokewa, kwanza ongeza anwani zinazosambaziwa kwenye orodha ya anwani. Ili kusambaza kwa anwani ya barua pepe, unahitaji pia kusanidi mipangilio ya seva ya barua pepe kabla.

Kusanidi Seva ya Barua

Kuweka Kabrasha Lililoshirikiwa La Mtandao

Kufanya Waasiliani Kupatikana

Hati za rangi haziwezi kusambazwa kwenye mashine nyingine ya faksi. Huchakatwa kama hati ambazo zilishindwa kusambazwa.

Kumbuka:
  • Kando na kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, unaweza kutumia Web Config kuweka mipangilio ya usambazaji ili kupokea faksi. Teua kichupo cha Fax > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti, kisha uweke mipangilio ya eneo la kusambazia kwenye Fax Output.

  • Unaweza kuchapisha na/au kuhifadhi faksi zilizopokelewa kwa wakati mmoja. Weka mipangilio kwenye skrini ya Fax Output iliyotajwa hapa juu.

  1. Teua Mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, kisha uteue Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi.

  2. Teua Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Hifadhi/Sambaza bila masharti.

    Wakati ujumbe unaonyeshwa, kagua maudhui, na kisha uguse Sawa.

  3. Unaweza kuweka mipangilio ya hadi maeneo matano ya kusambazia.

    Teua Sambaza.

    Teua Ndiyo. Ili uchapishe hati kiotomatiki wakati unazisambaza, chagua Ndiyo na Uchapishe badala yake.

    Mfikio > Ongeza Ingizo, kisha uteue maeneo ya kusambazia kutoka kwenye orodha ya waasiliani. Unaweza kubainisha hadi mafikio tano ya usambazaji.

    Gusa Funga ili ukamilishe kuchagua anwani za usambazaji,na kisha uguse Funga.

    Katika Chaguo Wakati Us'zaji Um'dikana, chagua kama unataka kuchapisha hati zilizopokewa au kuzihifadhi katika Kisanduku pokezi ya kichapishi wakati usambazaji unakosa kufaulu.

    Donoa Sawa.

    Muhimu:

    Wakati Kisanduku pokezi kimejaa, kupokea faksi hulemazwa. Unastahili kufuta hati kwenye kisanduku pokezi punde tu zinapoangaliwa. Idadi ya nyaraka ambazo zilishindwa kusambaza imeonyeshwa kwenye katika skrini ya nyumbani, kwa kuongezea kwenye kazi zingine zisizochakatwa.

    Kumbuka:

    Unaweza kuweka kichapishi kitume barua pepe kwa watu unaotaka kuwaarifu kuhusu matokeo ya usambazaji wa faksi wakati mchakato wa usambazaji ukikamilika. Ilivyo muhimu, teua Taarifa za Barua pepe, weka michakato na kisha uteue eneo unapotaka kutuma arifa kutoka kwenye orodha ya waasiliani.

  4. Teua Funga ili ukamilishe Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza bila masharti.

Kumbuka:
  • Hii hukamilisha uwekaji mipangilio ya usambazaji bila masharti ya kupokea faksi. Unaweza kuweka Mipangilio ya Kawaida ilivyo muhimu. Kwa maelezo, angalia ufafanuzi wa Mipangilio ya Kawaida katika menyu ya Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza.

  • Ikiwa umechagua kabrasha la kushiriki kwenye mtandao au anwani ya barua pepe kama mafikio wa usambazaji, tunapendekeza kwamba ujaribu kama unaweza kutuma picha iliyochanganuliwa hadi kwa mwishilio katika hali ya uchanganuzi. Teua Changanua > Barua pepe, au Changanua > Folda/FTP ya Mtandao kutoka kwenye skrini ya nyumbani, teua mafikio, na kisha anzisha utambazaji.