Haiwezi kupokea Faksi za Ukubwa wa A3

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Mpangilio wa chanMpangilio wa chanzo cha karatasi sio sahihi.

Suluhisho

Kagua kwamba mpangilio wa ukubwa wa karatasi wa chanzo cha karatasi ambacho kina karatasi ya A3 kimewekwa kwa A3, na kwamba chanzo cha karatasi kimewekwa kitumiwe na kipengele cha faksi. Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Mipangilio Chanzo Karatasi > Mipangilio ya Uchaguaji Oto > Faksi, na kisha ukague vyanzo vilivyowezeshwa vya karatasi.

A3 haijateuliwa kwenye Inapokea Ukubwa wa Karatasi.

Suluhisho

Teua Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio Msingi > Inapokea Ukubwa wa Karatasi na kisha uhakikishe kwamba A3 imeteuliwa. Menyu hii hukuruhusu kuweka ukuwa wa juu wa faksi ambao kichapishi kinaweza kupokea.