Ikiwa nozeli zimeziba, uchapishaji unakuwa fifu, mistati inaonekana, au rangi zisizotarajiwa zinaonekana. Wakati kuna tatizo kwenye ubora wa uchapishaji au unapochapisha kiwango kikubwa cha uchapishaji, tunapendekeza kutumia kipengele cha kuangalia nozeli. Ikiwa nozeli zimeziba, safisha kichwa cha kuchapisha.
Usifungue kifuniko cha kibweta cha wino au zima kichapishi wakati wa kusafisha kichwa. Ikiwa usafisha wa kichwa haujakamilika, huenda usiweze kuchapisha.
Kwa kuwa usafishaji wa kichwa cha chapisho hutumia wino kiasi, unaweza kutekelezwa wakati wino umepungua.
Kukausha kunasababisha kuzibika. Ili kuzuia kichwa cha chapisho kukauka, kila mara zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha
. Usichomoe kichapishi wakati nishati imewashwa.
Donoa Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa Matengenezo.
Donoa Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa.
Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuteua chanzo cha karatasi ambazo ulipakia karatasi tupu ya ukubwa wa A4.
Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini kuchapisha ruwaza ya kukagua nozeli.
Angalia ruwaza iliyochapishwa ili kuona iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimezibika.
Iwapo nozeli hazijazibika, donoa Sawa ili kukamilisha.
Sawa

NG

Iwapo nozeli zimezibika, donoa NG ili kusafisha kichwa cha chapisho.
Baada ya kukamilisha usafishaji, charaza tena ruwaza ya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa hakuna kuzibika. Iwapo bado nozeli zimezibika, rudia kusafisha kichwa na uendeshe ukaguzi wa nozeli.