> Kukarabati Kichapishi > Kuangalia Hali Ya Vitumika

Kuangalia Hali Ya Vitumika

Unaweza kuangalia viwango vya wino na maisha ya huduma ya kisanduku cha ukarabati katika paneli dhibiti au kwenye kompyuta.

Kukagua Viwango vya Wino

Donoa kwenye skrini ya nyumbani na uteue Vifaa vinavyotumika/Nyingine ili kuonyesha viwango vya wino vinavyokadiriwa kusalia.

Vibweta viwili vya wino mweusi vinasakinishwa kwenye kichapishi. Kwa kuwa vibweta vya wino vinabadilishwa kiotomatiki, unaweza kuendelea kuchapisha hata iwapo mojawapo inajikokota.

Unapotumia kiendeshi cha kichapishi, pia unaweza kuangalia kutoka kwenye kompyuta yako. Kwa watumiaji Windows, kumbuka kuwa unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki.

Kumbuka:

Unaweza kuendelea kuchapisha wakati ujumbe wa kupungua kwa wino umeonyeshwa. Badilisha katriji za wino unapohitajika.

Kuangalia Nafasi Inayopatikana kwenye Kisanduku cha Ukarabati

Donoa kwenye skrini ya nyumbani na uteue Vifaa vinavyotumika/Nyingine ili kuonyesha viwango vya nafasi inayopatikana kwenye kisanduku cha ukarabati.

Unapotumia kiendeshi cha kichapishi, pia unaweza kuangalia kutoka kwenye kompyuta yako. Kwa watumiaji Windows, kumbuka kuwa unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki.