> Maelekezo Muhimu > Maelekezo Muhimu ya Usalama > Kushughulikia Bidhaa Zinazotumika

Kushughulikia Bidhaa Zinazotumika

  • Kuwa makini unaposhughulikia katriji zilizotumika za wino, kwani kunaweza kuwa na wino kando ya lango la kutoa wino.

    • Wino ukikumwagikiwa kwenye ngozi, safisha sehemu hiyo vizuri ukitumia sabuni na maji.

    • Wino ukiingia ndani ya macho yako, yamwagie maji mara moja. Maumivu au matatizo ya kuona yakiendelea baada ya kuyamwagia maji, mtembelee daktari mara moja.

    • Wino ukiingia mdomoni mwako, mtembelee daktari mara moja.

  • Usifungue katriji ya wino na kisanduku cha ukarabati; la sivyo wino unaweza kuingia ndani ya macho yako au kukumwagikia kwenye ngozi.

  • Usitikise katriji za wino kwa nguvu; la sivyo wino unaweza kuvuja kutoka kwenye katriji ya wino.

  • Weka katriji za wino na kisanduku cha ukarabati mbali na watoto.

  • Usiruhusu ukingo wa karatasi kuteleza kwenye ngozi yako kwa sababu ukingo wa karatasi unaweza kukukata.