Anwani ya IP haijapangiwa ipasavyo.

Iwapo anwani ya IP iliyopangiwa kichapishi ni 169.254.XXX.XXX, na barakoa ndogo ni 255.255.0.0, huenda anwani ya IP isipangiwe kwa usahihi.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Mahiri > TCP/IP kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, kisha uangalie anwani ya IP na barakoa ndogo iliyopangiwa kichapishi.

Washa upya kipanga njia chako pasiwaya au weka upya mipangilio ya mtandao kwa kichapishi.

Iwapo mipangilio ya mtandao si sahihi, sanidi tena mipangilio ya mtandao wa kichapishi kulingana na mazingira ya mtandao.