Kusanidi Cheti cha Seva kwa ajili ya Kichapishi

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Network Security > SSL/TLS > Certificate

  4. Bainisha cheti cha kutumia katika Server Certificate.

    • Self-signed Certificate
      Cheti cha kujitilia sahihi mwenyewe kimezalishwa na kichapishi. Usipopokea cheti kilichotiwa sahihi na CA, teua hii.
    • CA-signed Certificate
      Ukipokea na kuleya cheti kilichotiwa sahihi na CA mapema, unaweza kubainisha hili.
  5. Bofya Next.

    Ujumbe wa uthibitishaji unaonyeshwa.

  6. Bofya OK.

    Kichapishi kimesasishwa.