> Maelezo ya Msimamizi > Kudhibiti Kichapishi > Kusanidi Usafishaji wa Kila Mara

Kusanidi Usafishaji wa Kila Mara

Unaweza kuweka mipangilio ya kufanya usafi kila mara kwenye kichwa cha kichapishi.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    Kichupo cha Device Management > Usafishaji wa Mara kwa Mara

  4. Teua chaguo kutoka kwenye orodha.

  5. Unapoteua Schedule, bainisha muda wa kufanya usafi kwenye orodha hiyo.

  6. Bofya OK.