Kuendesha Usafishaji wa Nishati

Kipengele cha Usafishaji wa Nishati kinaweza kuimarisha ubora katika hali zifuatazo.

  • Nozeli zinapoziba.

  • Ikiwa umeangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 3 na ukasubiri kwa muda wa saa 12 bila kuchapisha lakini bado ubora wa chapsiho haukuimarika.

Kabla ya kuendesha kipengele hiki, tumia kipengele cha ukaguaji nozeli na ukague kama nozeli zimeziba, soma maagizo yafuatayo, na kisha uendeshe Usafishaji wa Nishati.

Muhimu:

Usafishaji wa Nishati hutumia wino mwingi sana kuliko usafishaji wa kichwa.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Usafishaji wa Nishati.

  3. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuendesha kipengele cha Usafishaji wa Nishati.

  4. Baada ya kuendesha kipengele hiki, endesha ukaguaji nozeli ili kuhakikisha nozeli hazijaziba.

    Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuendesha ukaguzi wa nozeli, tazama maelezo husiani hapa chini.

Muhimu:

Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kuendesha Usafishaji wa Nishati, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uchapishe ruwaza ya uangaliaji nozeli tena. Endesha Usafishaji Kichwa cha Chapa au Usafishaji wa Nishati tena kwa kutegemea ruwaza iliyochapishwa. Ikiwa ubora bado hajuaimarika, wasiliana na timu ya usaidizi ya Epson.

Kumbuka:

Pia unaweza kuendesha usafishaji wa nishati kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi.

  • Windows

    Kichupo cha Utunzaji > Usafishaji wa Kichwa cha Kuchapisha > Usafishaji wa Nishati

  • Mac OS

    Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Printa na Vichanganuzi (au Chapisha na Uchanganue, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazajo > Matumizi > Fungua Matumizi ya Printa > Usafishaji wa Kichwa cha Kuchapisha > Usafishaji wa Nishati