> Katika Hali Hizi > Kuwuka Upya Muunganisho wa Mtandao > Kufanya Mipangilio ya Wi-Fi kutoka kwenye Paneli ya Kudhibiti > Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma (WPS)

Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma (WPS)

Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kiotomatiki kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.

  • Kipanga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).

  • Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Ikiwa huwezi kupata kitufe au unasanidi kwa kutumia programu, tazama hati iliyotolewa kwa kipanga njia pasiwaya.

  1. Teua kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).

  3. Bonyeza kitufe cha OK.

    Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Teua Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.

  4. Teua Sukuma Kitufe cha Usanidi (WPS).

  5. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

    Ukitaka kuangalia hali ya muunganisho wa mtandao ya kichapishi baada ya kukamilisha kusanidi, angalia kiungo cha maelezo husiani kilicho hapa chini kwa maelezo.

    Kumbuka:

    Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanga njia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.