Kufanya Mipangilio kwa Msimbo wa PIN Sanidi (WPS)

Unaweza kuunganisha kiotomatiki kwenye kipanga njia pasiwaya kwa kutumia msimbo wa PIN. Unaweza kutumia mbinu hii kuweka ikiwa kipanga njia pasiwaya kina uwezo wa WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa). Tumia kompyuta kuingiza msimbo wa PIN katika kipanga njia pasiwaya.

  1. Teua kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).

  3. Bonyeza kitufe cha OK.

    Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Teua Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.

  4. Teua Nyingine > Usanidi Msimbo PIN (WPS).

  5. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

    Ukitaka kuangalia hali ya muunganisho wa mtandao ya kichapishi baada ya kukamilisha kusanidi, angalia kiungo cha maelezo husiani kilicho hapa chini kwa maelezo.

    Kumbuka:

    Tazama waraka uliotolewa kwa kipanga njia pasiwaya chako kwa maelezo kuhusu kuweka msimbo wa PIN.