Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio Msingi
Mipangilio Msingi
Mwangaza wa LCD
Rekebisha mwangaza wa skrini ya LCD.
Kipima Saa ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Ongezeko lolote litaathiri ufanisi wa nishati ya bidhaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Ondoa Mipangilio Yote
Huweka upya Mipangilio Msingi kwa chaguo-msingi yake.