Hakikisha kuwa umesajili ukubwa na aina ya karatasi kwenye skrini inayoonyeshwa unapochomeka kaseti ya karatasi. Printa hukujulisha wakati maelezo yaliyosajiliwa na mipangilio ya kuchapisha inatofautiana. Hii hukuzuia kupoteza karatasi na wino kwa kuhakikisha kwamba huchapishi kwenye ukubwa usiofaa wa karatasi au kuchapisha kwa rangi isiyofaa kutoka na kutumia mipangilio ambayo hailingani na aina ya katarasi.

Iwapo ukubwa na aina ya karatasi inayoonyeshwa ni tofauti na karatasi iliyopakiwa, teua kipengee ambacho unataka kubadilisha. Iwapo mipangilio inalingana na karatasi iliyopakiwa, funga skrini.
Unaweza kuweka mipangilio kwa urahisi kwa kusajili mkusanyiko unaotumika mara kwa mara wa ukubwa na aina ya karatasi kuwa unaopenda. Unaweza kuunda mipangilio ya karatasi kwa kuteua kuweka awali kulikosajiliwa. Ili kusajili mpangilio wa awali, teua Mip. ya Kar'si U'ipenda, teua > katika skrini inayofuata kisha ubainishe ukubwa na aina ya karatasi.
Iwapo hutaki kuonyesha skrini ya mpangilio wa karatasi kiotomatiki unapochomeka kaseti ya karatasi, kwenye skrini ya nyumbani teua Mipangilio > Mipangilio ya Printa > M'gilio Chanzo Karatasi > Usanidi wa Karatasi, na kisha uteue Zima.