> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Picha kutoka kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Kuchapisha Picha zilizo na Madokezo Yaliyoandikwa kwa mkono

Kuchapisha Picha zilizo na Madokezo Yaliyoandikwa kwa mkono

Unaweza kuchapisha picha kwenye kifaa cha kumbukumbu kwa matini au michoro iliyoandikwa kwa mkono. Hii hukuruhusu kuunda kadi asili kama vile kadi za Mwaka Mpya au kadi za siku ya kuzaliwa.

Kwanza teua picha na uchapishe kiolezo kwenye karatasi tupu. Andika au chora kwenye kiolezo na kisha ukitambaze kwa kichapishi. Kisha unaweza kuchapisha picha kwa madokezo na michoro yako ya binafsi.

Chapa mbalimbali > Kadi ya Salamu > Teua picha na Uchapishe Kiolezo

Muhimu:
  • Usiondoe kifaa cha kumbukumbu hadi umalize kuchapisha.

  • Hakikisha kuwa matini kwenye kiolezo yamekauka kabisa kabla ya kukiweka kwenye glasi ya kichanganuzi. Iwapo kuna madoa kwenye glasi ya kitambazaji, pia madoa yanachapishwakwenye picha.