Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha (Windows)

  1. Pakia karatasi ya ukubwa wa A4 kwenye kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda 2 wa Karatasi

  2. Nenda kwa dirisha la kiendeshi cha kichapishi.

  3. Bofya Ukaguzi wa Nozeli kwenye kichupo cha Utunzaji.

  4. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

    Muhimu:

    Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 2, subiri kwa angalau saa 6 bila kuchapisha kisha uangalie nozeli tena na urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi ukitumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati.