Karatasi Huingia kama Imeinama

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Eneo la usakinishaji halifai.

Suluhisho

Weka printa kwenye eneo tambarare na uitumie katika hali ya mazingira iliyopendekezwa.

Karatasi isiyokubaliwa inatumika.

Suluhisho

Tumia karatasi inayokubaliwa na hiki kichapishi.

Ushughulikiaji wa karatasi si sahihi.

Suluhisho

Fuata maagizo ya kushughilikia karatasi.

Karatasi imepakiwa visivyo.

Suluhisho

Weka karatasi ikiwa inaangalia upande unaofaa, na telezesha mwongozo wa kingo kando ya kingo ya karatasi.

Laha nyingi zimepakiwa kwenye kichapishi.

Suluhisho

Usiweke zaidi ya upeo wa idadi ya karatasi uliotajwa kwa karatasi. Kwa karatasi tupu, usiweke zaidi ya mstari unaoonyeshwa na alama ya pembetatu kwenye mwongozo wa kingo.

Mipangilio ya karatasi kwenye kichapishi si sahihi.

Suluhisho

Hakikisha mipangilio ya ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi inalingana na ukubwa halisi wa karatasi na aina ya karatasi iliyopakiwa kwenye kichapishi.

Karatasi huteleza endapo vumbi ya karatasi inanata kwenye rola.

Suluhisho

Safisha rola.