> Kukarabati Kichapishi > Kusafirisha na Kuhifadhi Kichapishi

Kusafirisha na Kuhifadhi Kichapishi

Wakati unahitaji kuhifadhi kichapishi au kukihamisha au kwa ukarabati, fuata hatua zilizo hapa chini za kupakia kichapishi.

Tahadhari:

Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

Muhimu:
  • Wakati unahifadhi au kusafirisha printa, usiinamishe, usiiweke wima, au kuigeuza upande wa chini kuangalia juu; la sivyo wino utavuja.

  • Wacha katriji ziliwa zimefungwa. Kuondoa katriji kunaweza kukausha kichwa cha kuchapisha na huenda kukazuia printa isichapishe.

  1. Zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha .

  2. Hakikisha taa ya nishati imezima, na kisha uchomoe waya ya nishati.

    Muhimu:

    Chomoa waya ya nishati wakati taa ya nishati imezimwa. La sivyo, kichwa cha kuchapisha hakitarudi kwenye mkao wake na wino utakauka, na huenda isiweze kuchapisha.

  3. Tenganisha kebo zote kama vile waya ya nishati na kebo ya USB.

  4. Hakikisha kwamba hakuna kadi ya kumbukumbu au kifaa cha nje cha USB kilichoingizwa.

  5. Ondoa karatasi zote kutoka kwa kichapishi.

  6. Hakikisha hakuna nakala za kwanza kwenye kichapishi.

  7. Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa. Linda kishikizi cha katriji ya wino kwenye kesi kwa kuambatisha nyenzo za ulinzi zilizoambatishwa uliponunua kichapishi upande wa juu kwa tepu.

  8. Funga kitengo cha kitambazaji.

  9. Andaa kupakua kichapishi kama inavyoonyeshwa hapa chini.

  10. Weka kichapishi kwenye sanduku lake kwa kutumia vifaa vya kukinga.

Wakati unatumia kichapishi wakati mwingine, hakikisha unatoa utepe unaoshikilia kishikio cha kubweta cha wino. Ikiwa ubora wa uchapishaji utapungua wakati ujao utakaochapisha, safisha na ulinganishe kichwa cha kuchapisha.