Epson Event Manager ni programu inayokuruhusu kudhibiti utambazaji kutoka paneli dhibiti na kuhifadhi taswira kwenye kompyuta. Unaweza kuongeza mipangilio yako mwenyewe kama mipangilio ya kabla, kama vile aina ya waraka, eneo la kabrasha la hifadhi, na umbizo la picha. Tazama msaada wa programu kwa maelezo ya kutumia vipengele.
Windows 10
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > Event Manager.
Windows 8.1/Windows 8
Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.
Windows 7/Windows Vista/Windows XP
Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > Epson Software > Event Manager.
Teua Nenda > Programu > Epson Software > Event Manager.