> Maelezo ya Bidhaa > Maelezo ya Programu > Programu ya Utambazaji > Programu ya Kudhibiti Kitambazaji (Epson Scan 2)

Programu ya Kudhibiti Kitambazaji (Epson Scan 2)

Epson Scan 2 ni kiendesha kitambazaji kinachokuruhusu kudhibiti kitambazaji. Unaweza kurekebisha ukubwa, mwonekano, uangavu, ulinganuzi, na ubora wa picha zilizotambazwa. Unaweza pia kuanzisha programu hii kutoka programu inayooambatana na utambazaji wa TWAIN. Tazama msaada wa programu kwa maelezo ya kutumia vipengele.

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue EPSON > Epson Scan 2.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.

  • Windows 7/Windows Vista/Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > EPSON > Epson Scan 2.

Kuanzia kwenye Mac OS

Teua Nenda > Programu > Epson Software > Epson Scan 2.