Kuonyesha Maelezo ya Kina ya Mtandao kwenye Paneli Dhibiti

Wakati kichapishi chako kimeunganishwa kwenye mtandao, pia unaweza kutazama maelezo mengine yanayohusiana na mtandao kwa kuteua menyu unazotaka kuangalia.

  1. Donoa Settings kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Teua Network Settings > Network Status.

  3. Ili kuangalia maelezo, teua menyu unazotaka kuangalia.

    • Wired LAN/Wi-Fi Status
      Huonyesha maelezo ya mtandao (jina la kifaa, muunganisho, nguvu ya ishara, anwani ya IP ya kupata, na zaidi) kwa miunganisho ya Ethaneti na Wi-Fi.
    • Wi-Fi Direct Status
      Huonyesha iwapo Wi-Fi Direct (AP Rahisi) imewezeshwa au kulemazwa kwa miunganisho ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).
    • Print Status Sheet
      Huchapisha laha la hali ya mtandao. Maelezo ya Ethaneti, Wi-Fi, Wi-Fi Direct (AP Rahisi) na zaidi yamechapishwa kwenye kurasa mbili au zaidi.