Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kifaa cha kumbukumbu.
Weka nakala za kwanza.
Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye kichapishi.
Teua Scan kwenye paneli dhibiti.
Teua Memory Device.
Iwapo utaambatisha vifaa anuwai vya kumbukumbu kwenye kichapishi, teua kifaa cha kumbukumbu ambacho taswira zilizotambazwa zinahifadhiwa.
Weka vipengee kwenye kichupo cha Scan, kama vile umbizo la kuhifadhi.
Chaguo za Utambazaji kwa Utambazaji kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Teua kichupo cha Advanced Settings, na kisha ukague mipangilio, na uibadilishe ikiwezekana.
Chaguo za Kina kwa Utambazaji kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Teua kichupo cha Scan tena kisha udonoe
.
Taswira zilizotambazwa zinahifadhiwa kwenye makabrasha “001” hadi “999” kwenye kabrasha la “EPSCAN”.
Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyotambazwa hautakuwa sawa na asili.