> Kutatua Matatizo > Huwezi Kutatua Tatizo Baada ya Kujaribu Suluhu Zote > Haiwezi Kutatua Matatizo ya Uchapishaji na Kunakili

Haiwezi Kutatua Matatizo ya Uchapishaji na Kunakili

Jaribu matatizo yafuatayo ili kuanza mwanzo hadi utatue tatizo.

  • Hakikisha kwamba umelinganisha aina ya karatasi iliyopakiwa kwenye kichapishi na aina ya karatasi iliyowekwa kwenye kichapishi na mipangilio ya aina ya karatasi kwenye kiendesha kichapishi.

    Mipangilio ya Ukubwa na Aina ya Karatasi

  • Tumia mipangilio ya ubora wa juu kwenye paneli dhibiti au kiendesha kichapishi.

  • Sakinisha tena vibweta wino ambavyo tayari vimesakinishwa kwenye kichapishi.

    Kusakinisha tena vibweta wino kunaweza kuondoa vitu vilivoziba nozeli ya kichwa cha kuchapisha na kuruhusu wino kusambaa taaribu.

    Hata hivyo, kwa sababu wino hutumika wakati kibweta wino kimesakinishwa tena, ujumbe unaokuuliza kubadilisha kibweta wino unaweza kuonyeshwa kwa kutegemea kiwango cha wino kinachobaki.

    Ni Wakati wa Kubadilisha Kibweta cha Wino

  • Linganisha kichwa cha kuchapisha.

    Kulinganisha Kichwa cha Kuchapisha

  • Angalia nozeli ili uone ikiwa nozeli za kichwa cha kuchapisha zimeziba.

    Ikiwa kuna sehemu ambazo hazipo kwenye ruwaza za kuangalia nozeli, huenda nozeli zimeziba. Rudia kusafisha kichwa na kuangalia nozeli kwa kupishana mara 2 na uangalie ikiwa kuziba huko kumeondolewa.

    Kumbuka kwamba usafishaji wa kichwa cha kuchapisha hutumia wino.

    Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha

  • Zima kichapishi na usubiri kwa angalau saa 6 na uangalie ikiwa imeacha kuziba.

    Iwapo tatizo ni kuziba, kuacha kichapishi kwa muda bila kuchapisha kunaweza kutatua tatizo hilo.

    Unaweza kuangalia vipengee vifafuatavyo wakati kichapishi kimezima.

  • Angalia kwamba unatumia kibweta wino halali cha Epson.

    Epson inapendekeza utumie vibweta wino halali vya Epson. Bidhaa hii inarekebisha rangi kulingana na vibweta wino halali, kwa hivyo kutumia bidhaa zisizo halali kunaweza kupunguza ubora wa chapisho.

    Misimbo ya Kibweta cha Wino

  • Angalia iwapo utepe nzito imechafuka.

    Ikiwa kuna uchafu uliopaka utepe nzito, pangusa uchafu huo kwa makini.

    Kusafisha Filamu Angavu

  • Hakikisha kwamba hakuna vipande vya karatasi vinavyosalia kwenye kichapishi.

    Unapoondoa karatasi, Usiguse utepe nzito kwa mikono yako ua karatasi.

  • Angalia karatasi.

    Angalia ikiwa karatasi imejikunja au imepakiwa huku upande unaochapishika ukielekea juu.

    Tahadhari za Kushughulikia Karatasi

    Karatasi Inayopatikana na Uwezo

    Aina Zisizopatikana za Karatasi

  • Hakikisha kwamba hutumii kibweta wino cha kizee.

    Kwa matokeo bora, Epson inapendekeza utumie kibweta kizima cha wino kabla ya tarehe iliyochapishwa kwenye kifurushi au ndani ya miezi sita baada ya kufungua kifurushi, muda wowote unaotangulia.

  • Ukizima kichapishi na kusubiri kwa angalau saa 6 na ubora wa chapisho bado haujaimarisha, endesha Usafishaji wa Nishati.

    Kuendesha Usafishaji wa Nishati

Ikiwa huwezi kutatua taizo kwa kuangalia suluhu zilizo hapa juu, unaweza kuhitaji kuomba ukarabati. Wasiliana na usaidizi wa Epson.