Kusajili VoIP Gateway <Epson Device Admin>

Sajili VolP gateway unayotaka kutumia ili kutuma na kupokea faksi za IP.

Teua Fax > IP-FAX Settings > VoIP Gateway Settings kutoka kwenye kiolezo cha usanidi, na kisha uweke usajili wa VoIP gateway pamoja na mipangilio mingine ya VoIP Gateway.

  1. Teua kipengee unachotaka kusajili kwenye orodha ya Registered VoIP Gateway, na kisha ubofye Edit.

    Skrini ya Registered VoIP Gateway inaonyeshwa.

  2. Teua kila kipengee.

    • Name
      Ingiza jina la VoIP gateway ukitumia hadi vibambo 30 vinavyoweza kuonyeshwa katika UTF-16. Hata hivyo, vibambo vya kudhibiti (0x00 hadi 0x1F na 0x7F) haviwezi kutumika.
    • IP Address
      Ingiza jina la mwenyeji au anwani ya IP ya VoIP gateway. Unaweza kuingiza vibambo 0 hadi 127 ambavyo vinaweza kuonyeshwa katika ASCII (0x20 hadi 0x7E). Hata hivyo, huwezi kutumia nafasi au vibambo vifuatavyo: "<>\^`{¦}
    • Port Number
      Ingiza nambari ya kituo ya VoIP gateway ukitumia nambari za baiti moja kati ya safu 1 hadi 65535.
  3. Bofya OK.

Kumbuka:
  • Ili kubadilisha maelezo ya usajili wa VoIP gateway, chagua kipengee ambacho ungependa kubadilisha kwenye orodha ya Registered VoIP Gateway, na kisha ubofye Edit.

  • Ili kufuta maelezo ya usajili wa VoIP gateway, chagua kipengee ambacho ungependa kufuta kwenye orodha ya Registered VoIP Gateway, na kisha ubofye Delete.

  • Ili kufuta maelezo yote ya usajili wa VoIP gateway, bofya Delete All kwenye orodha ya Registered VoIP Gateway.