Sehemu hii inakuletea utendakazi wa usalama wa Vifaa vya Epson.
|
Jina la kipengele |
Aina ya kipengele |
Unachofaa kuweka |
Unachofaa kuzuia |
|---|---|---|---|
|
Usanidi wa nenosiri la msimamizi |
Hufunga mipangilio ya mfumo kama vile usanidi wa muunganisho kwa mtandao au USB, usanidi wa kina kwa upokeaji/uwasilishaji au uhamishaji wa faksi na mipangilio chaguomsingi ya mtumiaji. |
Msimamizi huweka nenosiri kwenye kifaa. Unaweza kuweka au kubadilisha kutoka kwenye Web Config pamoja na paneli dhibiti. |
Zuia kusoma na kubadilisha bila idhini maelezo yaliyohifadhiwa kwenye kifaa kama vile Kitambulisho, nenosiri, mipangilio ya mtandao na waasiliani. Pia, punguza masafa mapana ya hatari ya usalama kama vile kuvuja kwa maelezo kwa mazingira ya mtandao au sera ya usalama. |
|
Sanidi kwa udhibiti wa ufikiaji |
Weka vikomo vya utendakazi unaoweza kutumiwa kwenye vifaa, kama vile chapisho, utambazaji, nakala na faksi kwa kila mtumaiji. Iwapo utaingia kwa kutumia akaunti ya mtumiaji iliyosajiliwa mapema, umeruhusiwa kutumia utendakazi fulani. Vilevile, baada ya kuingia kutoka kwenye paneli dhibiti, utaondolewa kiotomatiki iwapo hutakitumia kwa kipindi fulani cha muda. |
Sajili akaunti yoyote ya mtumiaji kisha uruhusu utendakazi unaotaka kuruhusu, kama vile nakala na utambazaji. Unaweza kusajili hadi akaunti 10 ya mtumiaji. |
Hatari ya kuvuja na utazamaji wa data bila idhini inaweza kupunguzwa kwa kuweka idadi ya chini ya utendakazi kwa mujibu wa maudhui ya biashara na jukumu la mtumiaji. |
|
Sanidi kwa ajili ya kioleosura cha nje |
Hudhibiti kioleosura, kama vile kituo USB kinachounganisha kwenye kifaa. |
Wezesha au ulemaze kituo cha USB cha kuunganisha vifaa vya nje kama vile kadi ya kumbukumbu ya USB na muunganisho wa USB kwenye kompyuta. |
|