Pia unaweza kusajili waasiliani kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi.
Fikia Web Config na uteue kichupo cha Scan/Copy au Fax > Contacts.
Teua idadi unayotaka kusajili, na kisha ubofye Edit.
Ingiza Name na Index Word.
Teua aina ya mafikio kama chaguo la Type.
Huwezi kubadilisha chaguo la Type baada ya usajili kukamilika. Iwapo unataka kubadilisha aina, futa mafikio na kisha usajili tena.
Ingiza thamani kwa kila kipengee, na kisha ubofye Apply.