Unaweza kutumia mbinu zozote kati ya zifuatazo kutambaza ukitumia kichapishi hiki.
Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kabrasha iliyosanidiwa awali kwenye mtandao.
Unaweza kutuma faili za picha zilizotambazwa kwa barua pepe moja kwa moja kutoka kwenye kichapishi kupitia seva ya barua pepe iliyosanidiwa mapema.
Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi.
Unaweza kuhifadhi taswira zilizotambazwa moja ka moja kwenye kifaa cha kumbukumbu kilichochomekwa kwenye kichapishi.
Unaweza kutuma taswira zilizotambazwa kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hadi huduma ya wingu ambayo imesajiliwa mapema.
Unaweza kuhifadhi taswira iliyotambazwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi, kwa kutumia kipengele cha WSD.
Unaweza kuhifadhi taswira zilizotambazwa moja kwa moja kwenye kifaa maizi kama vile simu mahiri au kompyuta kibao kwa kutumia programu ya Epson iPrint kwenye kifaa maizi.