Ufafanuzi huu ni mfano wa kuunda kabrasha lililoshirikiwa kwenye eneo kazi la mtumiaji anayeingia sasa kwenye kompyuta.
Mtumiaji anayeingia kwenye kompyuta na aliye na mamlaka ya msimamizi anaweza kufikia kabrasha la eneo kazi na kabrasha la waraka ambazo zipo kwenye kabrasha la Mtumiaji.
Weka usanidi huu wakati HURUHUSU kusoma na kuandika kwenye mtumiaji mwingine hadi kwenye kabrasha lililoshirikiwa kwenye kompyuta ya kibinafsi.
Eneo la kuunda kabrasha lililoshirikiwa: Eneo kazi
Njia ya kabrasha: C:\Users\xxxx\Desktop\tambaza_kabrasha
Kibali cha kufikia kupitia mtandao (Shiriki Vibali): Kila mtu
Kibali cha kufikia kwenye mfumo wa faili (Usalama): usiongeze, au kuongeza majina ya Mtumiaji/Kikundi ili kuidhinisha ufikiaji
Ingia kwenye kompyuta mahali ambapo kabrasha lililoshirikiwa linafaa kuundwa kwa akaunti ya mtumiaji ya mamlaka ya msimamizi.
Washa kichunguzi.
Unda kabrasha kwenye eneo kazi, na kidsha ulipe jina “tambaza_kabrasha”.
Kwa jina la kabrasha, ingiza kati ya vibambo 1 hadi 12 vya alfanumeriki. Iwapo kiwango cha kibambo cha jina la kabrasha kimezidishwa, unaweza kulifikia kawaida kwa mazingira tofauti.
Bofya kulia kwenye kabrasha, na kisha uteue Sifa.

Bofya Kushiriki Mahiri kwenye kichupo cha Kushiriki.

Teua Shiriki kabrasha hili, na kisha ubofye Vibali.

Teua kikundi cha Kila mtu cha Kikundi au majina ya mtumiaji, teua Ruhusu kwenye Badilisha, na kisha ubofye Sawa.

Bofya Sawa.
Teua kichupo cha Usalama.
Angalia kikundi au mtumiaji kwenye Kikundi au majina ya mtumiaji.
Kikundi au mtumiaji aliyeonyeshwa hapa anaweza kufikia kabrasha lililoshirikiwa.
Katika hali hii, mtumiaji anayeingia kwenye kompyuta hii na Msimamizi anaweza kufikia kabrasha lililoshirikiwa.
Ongeza kibali cha ufikiaji, ikiwezekana. Unaweza kuiongeza kwa kubofya Hariri. Kwa maelezo haya, tazama Maelezo Husiani.

Teua kichupo cha Kushiriki.
Njia ya mtandao ya kabrasha lililoshirikiwa inaonyeshwa. Hii inatumika wakati wa kusajili kwa mwasiliani wa kichapishi. Tafadhali iandike chini.

Bofya Sawa au Funga ili kufunga skrini.
Angalia iwapo faili inaweza kuandikwa au kusomwa kwenye kabrasha lililoshirikiwa kutoka kwenye kompyuta za watumiaji au vikundi vilivyo na kibali cha ufikiaji.