Unapoteua Tambua Otomatiki kama mpangilio wa karatasi, aina zifuatazo za ukubwa wa karatasi zinatambuliwa kiotomatiki.
Kuweka wima: A4, B5, A5, 16K*
Weka ukingo mrefu wa nakala asili kwenye lango la mlisho wa karatsi la ADF au upande wa kushoto wa glasi ya kichanganuzi.

Kuweka kimlalo: A3, B4, A4, B5, A5 (glasi ya kichanganuzi pekee), 8K*, 16K*
Weka ukingo mfupi wa nakala asili kwenye lango la mlisho wa karatasi la ADF au upande wa kushoto wa glasi ya kichanganuzi.

*: Karatasi inagunduliwa wakati Kipaumbele cha Ukubwa wa K imewezeshwa. Hata hivyo, inaweza kukosa kugunduliwa kutegemea kazi unazotumia. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kwa maelezo zaidi.
Ukubwa wa nakala asili zifuatazo unaweza kutotambuliwa sahihi. Iwapo ukubwa hautatambuliwa, weka ukubwa mwenyewe kwenye paneli dhibiti.
Nakala asili zilizoraruka, kujikunja, ulio na kasoro (iwapo nakala asili zimejikunja, kunjua mkunjo huo kabla ya kuweka nakala asili.)
Nakala asili zenye mashimo mengi ya kubana
OHPs, nakala asili zinazopitisha mwangaza, au nakala asili, au nakala asili zinazometameta