Unaweza kuonyesha skrini ili kuangalia kazi za faksi ambazo uchakataji wake umekamilika. Kazi zifuatazo zinaonyeshwa kwenye skrini yaukaguzi. Kutoka kwenye skrini hii, pia unaweza kuchapisha nyaraka ambazo bado hazijachapishwa, au unaweza kutuma upya nyaraka ambazo zimeshindikana kutumwa.
Kazi za faksi zilizopokewa zipo hapa chini
Bado haijachapishwa (Wakati kazi zimewakwa kuchapishwa)
Bado hazijahifadhiwa (Wakati kazi zimewekwa kuhifadhiwa)
Bado hazijasambazwa (Wakati kazi zimewekwa kusambazwa)
Kazi za faksi zinazoondoka ambazo zimeshindwa kutumwa (ikiwa umewezesha Hifadhi Data ya Kushindwa)
Fuata hatua za hapa chini ili kuangalia skrini ya ukaguzi.
Donoa Kazi/Hali kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa kichupo cha Hali ya Kazi, na kisha udonoe Inatumika.
Teua kazi unayotaka kukagua.