Kikasha pokezi/Siri

Unaweza kutafuta Kikasha pokezi/Siri kwenye Kasha la Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

Kisanduku pokezi na Vikasha vya Siri(Orodha)

Kisanduku pokezi na vikasha vya siri kwenye Kasha la Faksi > Kikasha pokezi/Siri.

Unaweza kuhifadhi hadi nyaraka 200 kwenye kikasha pokezi na kikasha cha siri kwa jumla.

Unaweza kutumia Kikasha pokezi kimoja na usajili hadi vikasha 10 vya siri. Jina la kikasha linaonyeshwa kwenye kikasha. Ya siri XX ni jina chaguo-msingi kwa kila kikasha cha siri.

Kisanduku pokezi na Vikasha vya Siri

Huonyesha orodha ya faksi zilizopokewa kwa jina la mtumiaji, tarehe zilipokelewa na kurasa. Iwapo Jina la Faili limewekwa kwenye Nyingine, jina la faili huonyeshwa badala ya jina la mtumaji.

Uhakiki:

Huonyesha skrini ya ukaguzi wa waraka.

Teua ili kuonyesha ukaguzi wa ukurasa.

skrini ya uhakiki wa ukurasa
  • : Hupunguza au kuongeza.

  • : Huzungusha picha upande wa kulia kwa digrii 90.

  • : Husogeza skrini katika mwelekeo wa vishale.

  • : Husonga kwa ukurasa wa awali au unaofuata.

Ili kuficha ikoni za operesheni, donoa mahali popote kwenye skrini ya uhakiki isipokuwa kwa ikoni. Donoa tena ili kuonyesha ikoni.

Endelea Kuchapisha:

Huchapisha waraka unaokagua kwanza. Unaweza kuweka mipangilio kama vile ya Nakala kabla ya kuanza kuchapisha.

Futa:

Hufuta waraka unaokagua kwanza.

Maelezo:

Huonyesha maelezo ya waraka uliochaguliwa kama vile tarehe na muda uliohifadhiwa na jumla ya idadi ya kurasa.

Tuma/Hifadhi:

Unaweza kutekeleza operesheni zifuatazo kwa waraka ulioteuliwa.

  • Tuma Faksi

  • Sambaza(Barua pepe)

  • Tuma mbele(Kabrasha la Mtandao)

  • Hifadhi kwenye Kumbukumbu

Unaweza kuteua PDF au TIFF kwenye Umbizo la Faili unapohifadhi au kusambaza waraka. Unapoteua PDF unaweza kuweka mipangilio ifuatayo kwenye Mipangiliuo ya PDF inavyohitajika.

  • Nenosiri la Kufungua Hati

  • Nenosiri la Vibali la Uchapishaji na Kuhariri

Wakati ujumbe Futa Ikikamilika unaonyeshwa, teua Washa ili kufuta faksi baada ya kukamilisha michakato kama vile Sambaza(Barua pepe) au Hifadhi kwenye Kumbukumbu.

Futa:

Hufuta waraka ulioteuliwa.

Nyingine:
  • Jina la Faili: Huweka jina la nyaraka iliyochaguliwa.

(Menyu ya Kasha)
Chapisha Zote:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huchapisha faksi zote kwenye kikasha. Kuteua Washa kwenye Futa Ikikamilika hufuta faksi zote wakati uchapishaji umekamilika.

Hifadhi Zote kwenye Kifaa cha Kumbukumbu:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Huhifadhi faksi zote kwenye vifaa vya kumbukumbu ya nje kwenye kikasha.

Unaweza kuteua PDF au TIFF kwenye Umbizo la Faili unapohifadhi au kusambaza waraka. Unapoteua PDF unaweza kuweka mipangilio ifuatayo kwenye Mipangiliuo ya PDF inavyohitajika.

  • Nenosiri la Kufungua Hati

  • Nenosiri la Vibali la Uchapishaji na Kuhariri

Kuteua Washa kwenye Futa Ikikamilika hufuta nyaraka zote wakati kuhifahi kumekamilika.

Futa Zote Zilizosomwa:

Hii huonyeshwa tu wakati kuna nyaraka kwenye kikasha. Hufuta nyaraka zote kwenye kisanduku.

Futa Zote Ambazo Hazijasomwa:

Hii huonyeshwa tu wakati kuna nyaraka kwenye kikasha. Hufuta nyaraka zote ambazo hazijasomwa zilizo kwenye kikasha.

Futa Zote:

Hii inaonyeshwa tu wakati kuna nyaraka za faksi zilizohifadhiwa kwenye kikasha. Hufuta faksi zote kwenye kikasha.

Mipangilio:

Vipengee vifuatavyo vinaonyeshwa unapoteua Kisanduku pokezi > Menyu ya Kasha > Mipangilio.

  • Chaguo wakati kumbukumbu imejaa: Teua chaguo moja ili kuchapisha au kukataa faksi zinazoingia baada ya Kikasha pokezi kujaa.

  • Mipangilio ya Nenosiri la Kisanduku pokezi: Unaweza kuweka nenosiri au kulibadilisha.

  • Futa Faksi Zilizopokewa Kiotomatiki: Kuteua Washa hufuta nyaraka za faksi zilizopokelewa kwenye kikasha kiotomatiki baada ya kipindi cha muda. Wakati Fuata Mipangilio ya Faksi imeteuliwa, mipangilio ifuatayo hutumika.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Mipangilio ya Hifadhi/Sambaza > Mipangilio ya Kawaida > Mipangilio ya Kisanduku ya Kufuta Hati

Vipengee vifuatavyo vinaonyeshwa unapoteua kikasha cha siri na kuteua Menyu ya Kasha > Mipangilio.

  • Jina: Ingiza jina la kikasha cha siri.

  • Nywila ya Kufungua Kikasha: Unaweza kuweka nenosiri au kulibadilisha.

  • Futa Faksi Zilizopokewa Kiotomatiki: Kuteua Washa hufuta nyaraka za faksi zilizopokelewa kwenye kikasha kiotomatiki baada ya kipindi cha muda.

Futa Kasha:

Kipengele hiki kinaonyeshwa tu wakati unachagua kisaduku cha siki na uchague Menyu ya Kasha. Hufuta mipangilio ya sasa ya Visaduku vya Siri na hufuta hati zote zilizohifadhiwa.

Nakala:

Weka idadi ya nakala za kuchapisha.

Mipangilio ya Chapa:

Unaweza kuweka vipengee vifuatavyo.

Pande 2:

Huchapisha kurasa anuwai za faksi zilizopokewa katika pande zote za karatasi.

Pambizo ya Kufunga

Kumalizia:
  • Kumalizia

  • Toa Karatasi

  • Bana kwa stepla

  • Toboa

Trei ya Towe:

Teua trei ya towe.

Teua Ukurasa:

Teua kurasa unazotaka kuchapisha.

Futa Ikikamilika:

Hii ikiteuliwa, waraka ulioteuliwa unafutwa uchapishaji unapokamilika.

Anza Kuchapisha:

Huchapisha waraka ulioteuliwa.