Kichupo cha Kukamilisha Windows (Wakati Kikamilishi cha Kijitabu Kimesakinishwa)

Panga:

Upangaji Hamishi:

Huondoa kila seti ya nakala. Unaweza kuteua chaguo hili tu wakati umeteua Uteuzi Otomatiki au Trei Kamilishi kuwa mpangilio wa Trei ya Zao.

Bana kwa stepla:

Teua eneo la stepla.

Toboa:

Teua eneo la shimo linalotobolewa. Huonyeshwa wakati kitengo cha kutoboa kimesakinishwa.

Kunja/Stichi ya Seruji:

Teua iwapo unataka kukunja au kukunja na kutaraza machapisho. Unaweza kuweka ukingo wa kuunganisha na ukingo wa kufunga kwenye skrini ya mipangilio ya kuunganisha.

Booklet Settings:

Unaweza kuweka aina ya kuunganisha, ukingo wa kufunga, uchapishaji wa kifuniko, kuongeza nambari za ukurasa, na kadhalika.