> Maelezo ya Bidhaa > Maelezo ya Programu > Programu ya Kuchapisha > Programu inayoweza kuchapisha Lugha ya PCL (Kiendeshi cha Kichapishi cha PCL)

Programu inayoweza kuchapisha Lugha ya PCL (Kiendeshi cha Kichapishi cha PCL)

Kiendeshi cha Kichapishi cha PCL huruhusu kichapishi kupokea na kufasiri maagizo ya uchapishaji kwenye lugha ya ufafanuzi wa ukurasa kilichotumiwa kutoka kwenye kompyuta na kuchapisha ipasavyo. Hii ni nzuri kwa uchapishaji kutoka programu za kawaida kama Microsoft Office.

Kumbuka:

Mac OS haiauniwi.

Unganisha kichapishi kwenye mtandao sawa kama kompyuta, na kisha ufuate utaratbu hapa chini ili kusakinisha kiendeshi cha kichapishi.

  1. Pakua faili zinazoweza kutekelezwa za kiendeshi kutoka kwa tovuti ya auni ya Epson.

    http://www.epson.eu/Support (Ulaya peke yake)

    http://support.epson.net/

  2. Bofya mara mbili kwa faili zinazoweza kutekelezwa.

  3. Fuata maagizo ya skrini kwa usakinishaji unaosalia.

    Kumbuka:

    Iwapo unatumia kompyuta ya Windows na huwezi kupakua kiendeshi kutoka kwenye tovuti, kisakinishe kutoka kwa diski ya programu ambayo ilikuja na kichapishi. Fikia “Driver\PCL Universal”.