> Maelezo ya Bidhaa > Sifa za Fonti > Fonti za Msimbo wa Mwambaa za Epson BarCode Fonts (Windows Pekee) > MaMadokezo kuhusu kuweka na kubadili umbizo la misimbo ya mwambaa

MaMadokezo kuhusu kuweka na kubadili umbizo la misimbo ya mwambaa

Tafadhali kumbuka kwamba unapoweka au kubadilisha vibambao vya msimbo wa mwambaa:

  • Usitumie michoro au umbizo la vibambo maalum, kama vile kukolea, italiki au kupiga mistari.

  • Chapisha misimbo ya mwambaa katika nyeusi na nyeupe pekee.

  • Unapozungusha vibambo, bainisha pembe za kuzungusha za 90˚, 180˚ na 270˚ pekee.

  • Zima mipangilio yote ya uwekaji vibambo na nafasi ya maneno kiotomatiki kwenye programu yako.

  • Usitumie vipengele kwenye programu yako vinavyopanua au kupunguza ukubwa wa vibambo katika mwelekeo ya wima au wa mlalo pekee.

  • Zima vipengele vya programu yako vya kurekebisha kiotomatiki wa tahajia, sarufi, nafasi n.k.

  • Ili kuweza kutofautisha kati ya misimbo ya mwambaa na matini mengine kwenye waraka wako, weka programu yako ionyeshe ishara za matini, kama vile alama za aya, vichupo, n.k.

  • Kwa sababu vibambo maalum kama vile mwambaa wa Kuanza na mwambaa wa Kukoma huongezwa wakati Epson BarCode Font imechaguliwa, msimbo wa mwambaa unaotoakana nazo unaweza kuwa na vibambo zaidi kuliko ingizo asili.

  • Kwa matokeo bora, tumia ukubwa wa fonti zilizopendekezwa kwenye “Sifa za Epson BarCode Font” kwa Epson BarCode Font unayotumia. Misimbo ya mwambaa katika ukubwa mwingine huenda usisomeke na visomaji vyote misimbo ya mwambaa.

  • Teua Rekebu-kijivu kwenye Mipangilio ya Kuchapisha na Wastani au Juu kwenye Ubora.

Kumbuka:

Kwa kutegemea uzito wa chapisho au ubora au rangi ya karatasi, misimbo ya mwambaa huenda isisomeke na visomaji vyote ya msimbo wa mwambaa. Chapisha sampuli na uhakikishe kwamba msimbo wa mwambaa unaweza kusomwa kabla ya kuchapisha kwa wingi zaidi.