Fonti za Msimbo wa Mwambaa za Epson hukuruhusu kuunda kwa urahisi aina nyingi ya misimbo ya mwambaa.
Kikawaida, uundaji wa msimbo wa mwambaa ni mchakato mgumu unaohitaji ubainishe misimbo ya amri, kama vile mwambaa wa Kuanza, mwambaa wa Kukoma na OCR-B, pamoja na misimbo ya mwambaa, vibambo vyenyewe. Hata hivyo, Fonti za Msimbo wa Mwambaa za Epson zimeundwa ili kuongeza misimbo kama hiyo kiotomatiki, hivyo kukuruhusu kuchapisha misimbo ya mwambaa kwa urahisi katika viwango mbalimbali vya msimbo wa mwambaa.