Kudayo Kutuma Faksi kutoka kwa Huduma ya Simu ya Nje

Unaweza kutuma faksi kwa kudayo ukitumia simu iliyounganishwa unapotaka kuzungumza kwenye simu kabla ya kutuma faksi, au wakati mashine ya faksi ya mpokeaji haibadilishi kwa faksi kiotomatiki.

  1. Inua mkono wa kifaa cha simu na kisha udayo nambari ya faksi ya mpokeaji kwa kutumia simu.

    Kumbuka:

    Mpokeaji anapojibu simu, unaweza kuzungumza na mpokeaji.

  2. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

  3. Weka mipangilio inayofaa kwenye Mipangilio ya Faksi.

    Mipangilio ya Faksi

  4. Unaposikia toni ya faksi, donoa kitufe cha , na kisha ukate simu.

    Kumbuka:

    Wakati nambari inapigwa kupitia simu iliyounganishwa, huwa inachukua muda mrefu kutuma faksi kwa sababu kichapishi hufanya utambazaji na utumaji wakati mmoja. Wakati unatuma faksi, huwezi kutumia vipengele vingine.